Ubalozi ulitembelea Mtambo wa Kusafisha Maji ya Bwawa kwa ajili ya Matumizi ya Kunywa na Majumbani uliotengnezwa na Kusimamiwa na Kampuni ya AMENHYD uliyopo Wilaya Akbou Mkoani Bejaia. Mtambo huo wa kisasa una uwezo wa Kusambaza Maji kwa zaidi ya umbali wa Kilomita 300. Aidha, Kampuni hiyo ya AMENHYD inatarajiwa kwenda Tanzania kwa ajili ya Kukutana na Mamlaka za Maji nchini na Kuangalia namna bora ya Kushirikiana katika Sekta hiyo pamoja na Kubadilishana Uzoefu ili Kuwasaidia Watanzania Kuondokana na Kero ya Ukosefu wa Maji Safi na Salalama.