Mhe. Balozi Maj Gen (Mst) Jacob Gideon Kingu alifanya Ziara ya Kakazi Mkoani Oran na Kutemblea Complex ya TOSYALI. Complex hiyo ni Uwekezaji wa Kampuni ya Kituriki ambayo imejikita katika Utengenezaji wa Bidhaa za Chuma.
Mheshimiwa Balozi alikutana na Kuzungumza na Mwekezaji huyo Bw Alp Topcuoglu Kuona Umuhimu wa Kuwekeza nchini Tanzania. Complex ya TOSYALI inatajwa kuwa ndio Complex kubwa Barani Afrika.



