Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania nchini Algeria, Mhe. Sidi Mohamed Abdallah, mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Algiers mnamo tarehe 17 Juni, 2026, kwa ajili ya kutambulishana na kuzungumzia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers unaiwakilisha pia Tanzania nchini Mauritania.