Algeria ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta ya kilimo hususan katika eneo la umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu bora, matumizi ya teknolojia, uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, tafiti na kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuongeza uzalishaji.

Hayo yamesemwa na Mhe. Youcef  Chorfa, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Vijiji wa Algeria wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na Mhe. Balozi Iman Njalikai katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Algiers Tarehe 16 Oktoba 2024.