Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Niger nchini Algeria, Mhe. Malam Manzo Aminou, mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jijini Algiers mnamo tarehe 11 Juni, 2026, kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers unaiwakilisha pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Niger.
