Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tunisia nchini Algeria, Abdelijalil Ben Rabeh, mara baada ya kukutana jijini Algiers mnamo tarehe 11 Juni, 2026, kwa ajili ya kutambulishana na kuzungumzia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers unaiwakilisha pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Tunisia.