Mhe. Balozi Meja Jenerali (Mst) Jacob Gideon Kingu alikutana na Kufanya Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje Jijini Algiers tarehe 13 Agosti, 2023. Katika Kikao hicho, Mhe. Balozi alitanguliza Shukurani za dhati kwa Mhe. Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Serikali ya Algeria kwa Ushirikiano Mzuri waliompatia katika Kutekeleza Majukumu yake ya Kidiplomasia katika Kipindi cha Utumishi wake Nchini Algeria. Aidha, Mhe. Balozi alimuaga Rasmi Mhe. Waziri na kumueleza kuwa amemaliza muda wake wa utumishi na anarudi nyumbani Tanzania. Kwa upande wake Mhe. Waziri Ahmed Attaf alimpongeza Mhe. Balozi Kingu kwa Kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi kifupi cha muda wake nchini Algeria na Kupaisha Ushirikiano wa Nchi hizi mbili ikiwemo Mafanikio ya Ziara Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb), Mhe. Dkt, Stergomena L. Tax na Mkutano Mkuu wa Tano wa Tume ya Kudumu ya Ushirikiano uliyofanyika Jijjini Algiers tarehe 30 Julai, hadi 01 Agosti, 2023. Mhe. Waziri Attaf amemhakikishia Mhe. Balozi kuwa Algeria itaendelea Kushirikiana na Tanzania katika Maeneo yote muhimu kwa maslahi ya Watu wetu.