Balozi Njalikai amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam chini ya Prof. Nelson Boniface, Naibu Makamu wa Chuo anayeshughulikia tafiti.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 30 Januari 2025 Chuoni hapo, yamelenga kuanzisha ushirikiano kati ya UDSM na Vyuo Vikuu vya Algiers 2 & 3 vya Algeria.
Ushirikiano huo utawezesha uendeshaji wa kozi, programu, tafiti, ubadilishanaji wa wakufunzi na utekelezaji wa miradi ya pamoja kwa maslahi ya pande zote mbili.



