Pamoja na Juhudi za Kuimarisha Mashirikiano ya Kidiplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria umelipa Kipaumbele Suala la Kuhamisha Maarifa na Teknolojia kwenda Tanzania. Katika Kufanikisha Mpango huo, Mheshimiwa Balozi amewatembelea Wanafunzi wa Kitanzania nchini Algeria wanaosoma katika Mikoa ya Annaba na Constantine na kuwataka wasome kwa Bidii na Kurudi Nyumbani baada ya Kuhitimu Masomo yao.

Mheshimiwa Balozi pia amewasikiliza Wanafunzi hao juu ya Changamoto zinazowakabili katika Masomo yao hususan katika kipindi hiki cha COVID 19 na kutatua baadhi ya Changamoto hizo.