Katika Kuendeleza na Kukuza Mashirikiano ya Kiuchumi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mheshimiwa Balozi Mag Gen. Jacob G. Kingu amekutana na Kufanya Mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Algeria, Mheshimiwa Kamel REZIG. Viongozi hao wamejadili kwa Upana kuhusu Umuhimu wa Kuimarisha Mashirikiano ya Kiuchumi baina ya Nchi mbili ikiwa ni pamoja na Kusainiwa kwa "Joint Permanent Commission" (JPS) pamoja na Kuanzishwa kwa Baraza la Wafanyabiashara wa Algeria na Tanzania ambalo litawawezesha Wafanyabiashara wa Nchi zote mbili Kufahamiana na vile vile Kuzitumia Fursa zilipo katika Maeneo mbali mbali ya Biashara na Uwekezaji. Aidha, Mheshimiwa Waziri amemueleza Mheshimiwa Balozi kuwa tayari ameshatoa Maelekezo kwa Rais wa "Chamber of Commerce" Kuanzisha Baraza la Wafanyabiashara wa Algeria na Tanzania na Kuushirikisha Ubalozi ili kuanza Kazi Mapema iwezekanavyo.


