Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Kingu alishiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji Algiers lililoandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Uwekezaji cha Waarabu wa Afrika.

Kongamano hilo lilijumuisha Wadau Masuala ya Uchumi na Fedha, Mabalozi na  Wataalamu wa Forodha. Aidha, Mheshimiwa Balozi alifanya Mahojiano na Televisheni ya Ennahar  na Kueleza frusa za Uwekezaji na Biashara zilizopo nchini Tanzania katika Eneo la Nishati, Kilimo na Utalii.

Pichani Mheshimiwa Balozi akipata Maelezo na Motisha zinazotolewa na Forodha ya Algeria kwa Bidhaa zinazozlishwa Nchni Algeria kwenda nje ya Nchi.