Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria kwa Kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Waarabu wa Afrika (CAAID) ulindaa Kongamano la Wawekezaji na Wafanyabiashara Waalgeria. Kongamano hilo limewapa nafasi Wadau hao Kufahamu fursa za Biashara na Uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
Katika Kongamano hilo, Mheshimiwa Balozi amewaeleza Wafanyabiashara na Wawekezaji Bidhaa za Bora za Kilimo wanaweza kuagiza kutoka Tanzania kama vile Korosho na Kahawa. Uwekezaji katika Sekta ya Hoteli na Madini pamoja na Taratibu za Uwekezaji na Mifumo ya Kibenki. Kongamano hilo limefanikiwa Kuwahamasisha Wafanyabiashara Kwa wingi zaidi kufika Ubalozini kwa ajili ya Kupata Mwongozo wa Kufanya Biashara na Tanzania.


