Mnamo Tarehe 09 Agosti 2020, Mheshimiwa Balozi na Familia yake waliwasili Kituoni Nchini Algeria kwa ajili ya Kuanza Majukumu yake ya Ubalozi. Mheshimiwa Balozi alipokelewa na Mabalozi wa Wakilishi wa Jumuiya  ya Afrika Mashariki, SADC, Umoja wa Mabalozi wa Afrika pamoja na Viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria.