Mheshimiwa Balozi Omar Yussuf Mzee akiambatana na Mabalozi wa Nchi mbali mbali na Jumuiya za Kimataifa waliopo nchini Algeria wametembelea Kambi za Wakambizi wa Sahara Magharibi zilizopo Mkoani Tindouf nchini Algeria. Katika Ziara hiyo, Waheshimiwa Mabalozi walipata fursa ya Kutembelea Miradi ya UNESCO, UNHCR, WFP pamoja na Miradi ya Taasisi zisizo za Kiserikali ambayo imelenga kuboresha Mazingira na Maisha ya Wakimbizi hao ikiwemo, upatikanaji wa Maji Safi, Huduma za Afya, Elimu ya Msingi na Mafunzo ya Ujasiri Amali.
Wakimbizi wa Polisari wameendelea Kuuomba Umoja wa Mataifa na Taasisi za Kiserikali kuutafutia ufumbuzi wa Kudumu Mgogoro wao na Morocco ili waweze kurudi katika ardhi yao na Kufanya Shughuli zao za Kimaendeleo. Aidha, wamesisitiza kuwa Sahara Magharibi ndio Taifa pekee barani Afrika ambalo bado linaendelea kutawaliwa.


