Katika Kusimamia Maalekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC waliopo nchini Algeria wamesimama Kutoa Tamko la Pamoja kupinga Vikwazo vya Kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe na Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani.
Tamko hilo lilisomwa mbele ya Waandishi wa Habari na Mheshimiwa Balozi Omar Yussuf Mzee Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria.
