Ubalozi ulishiriki kwenye Maonesho ya 13 ya Kimataifa ya Utalii yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mohamed Benahmed (CCO), Jijini Oran kuanzia tarehe 22 hadi 25 Februari, 2023. Maonesho yalishirikisha takriban Kampuni 200 za Utalii, Mahoteli na Wafanyabishara mbalimbali. Zaidi ya watu 8,000 wakiwemo wenye Mabanda ya Maonesho na wageni waliotembelea kwenye Mabanda hayo. Nchi zilizoshiriki (Exhibitors) kwenye Maonesho hayo ni Tanzania, Senegal, Tunisia, Misri na China. Aidha, Ubalozi wa Zimbabwe ulitembelea Maonesho kama wageni waalikwa (Visitors).

 

Aidha, Mawakala wa Utalii wawili kutoka Tanzania walishiriki kwenye Maonesho hayo. Mawakala hao ni Kenzan Wildlife Safaris (Bwana Philip Mbotto kutoka Tanzania Bara na Palm Tours (Bwana Juma Khalid) kutoka Zanzibar. Ubalozi unapenda kutoa wito kwa Wadau wa Utalii Tanzania Kushiriki katika Majukwaa ya Kimataifa ya Utalii yanayofanyika nchini Algeria ili kuongeza idadi ya Watalii kutoka Nje.