Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria umeipa Kipaumbele Diplomasia ya Kiuchumi. Mheshimiwa Balozi ameendeleza Mazungumzo na Meneja Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji cha Waarabu wa Afrika Bwana Mohamed Amine Boutalbi juu ya Kuanziasha Mashirikiano ya Pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania ili Kufungua Milango ya Mashirikiano ya Kiuchumi baina ya nchi zao mbili. 

Bwana Amine ameeleza kuwa Ujumbe wake upo tayari kwenda Tanzania baada ya hali ya Corona Kutengemaa na Vile vile katika Kituo chao Uwekezaji kiko njia Kuzindua Chanel yake ambayo pia itatumika kutangaza fursa za Biashara na Uwekezaji zilizopo Tanzania  kwa lengo la Wafanyabiashara wa Algeria kulifahamu zaidi Soko la Tanzania.