Mhe. Balozi Mej Jen. (Mst) Jacob Kingu alifanya Mazungumzo na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Afrika Kaskazini kutoka Kampuni ya HIKMA, Bibi Sihem SAADA alipomtembelea Ubalozini Jijini Algiers tarehe 31 Januari, 2023. Hikma ni Kampuni ya Kimataifa ya Uzalishaji wa Dawa za Binadamu ambayo imeekeza zaidi kwenye Uzalishaji wa “Generic” nchini Algeria.
Katika Kikao hicho Bi. Sihem alielezwa kuhusu fursa zilizopo nchini Tanzania kwenye upande wa Sekta ya Dawa za Binadamu na Vifaa Tiba ikiwemo Soko la Uhakika pamoja na Sera nzuri za Uwekezaji zinazosimamiwa na Serikali ya Awamu ya sita (6). Hivyo ameiomba Kampuni hiyo Kuangalia uwezekano wa Kuwekeza nchini Tanzania na Kusajili Dawa zao kwenye Mamlaka ya TMDA.

