Mnamo tarehe 08 Februari, 2022, Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Kingu alikutana na Kufanya Mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni ya “Golden Moment” ya Algeria ambayo inafanya Kazi Kusafirisha Watalii kutembelea nchi mbali mbali duniani.
Katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Yassir TAIBI alieka wazi kuwa Kampuni yao imeratibu Kutembelea Vivutio vya Utalii wa Tanzania na Kuandaa “Documentary” itakayorushwa katika Televisheni ya Algeria na Mitandao Kijamii kwa lengo la Kuutangaza Utalii wa Tanzania nchini Algeria na Kuimarisha Mashirikiano ya Sekta ya Utalii kati ya Nchi zetu mbili.
Ziara hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka, 2022.

