Mheshimiwa Balozi amekutana na Kufanya Mazungumzo na Bwana Noucer, Mwekezaji katika Sekta ya Nishati na Mmiliki wa Kiwanda cha Aures Solaire kinachoshughulika na Uzalishaji wa Vigae vya Umeme (Solar Panel). Bwana Noucer amemuelezea Mheshimiwa Balozi kuwa Aures Solaire inazalisha Solar Panel za Kisasa na zenye ubora na uimara wa  hali ya juu. 

Baada ya Kumkaribisha, Mheshimiwa Balozi amumueleza Bwana Noucer kuwa moja ya Sekta inayokua nchini Tanzania ni Sekta ya Nishati. Hivyo Kampuni ya Aures Solaire inayofursa kubwa ya kwenda Kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kuanzia pia inaweza ikaanza Kushiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba saba kwa ajili ya Kuonesha Bidhaa zao na Kufungua Tawi la Usambazaji.