Mheshimiwa Balozi amekutana na Kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusafirisha Watalii ya Alltour Bwana Salim Belhaine. Kampuni ya Alltour ni Miongoni mwa Makampuni ya Kialgeria ambayo tayari yameshaanza Kupeleka Wageni nchini Tanzania kuanzia mwaka 2019.
Katika Mazungumzo yao, Wamezungumzia namna ya Kuimarisha Mashirikiano ya Utalii katika Mazingira ya Corona pamoja na Kuutangaza Utalii wa Tanzania nchini Algeria ikiwa ni pamoja na Kuandaa ziara ya Makampuni ya Utalii kwenda nchini Tanzania ili Kujionea Vivutio vya utalii na Baadae kuja Kuvitangaza nchini Algeria.
