Katika ziara yake Mheshimiwa Balozi Mej. Gen Jacob Gideon Kingu, Mkoani Constantine amekutana na Katibu wa Shirikisho la Taifa la Wamiliki wa Hoteli Bwana Abdelouhab Boulfekhad ambae pia ni Mmiliki wa Hoteli ya Hocine na Chuo cha Utalii Binafsi Mkoani Constantine.
Viongozi hao walizungumza kuhusu fursa za Uwekezaji nchini Tanzania kwenye Sekta ya Utalii na Viwanda pamoja na Kubadilishana Uzeofu katika Sekta hizo.
