Mhe. Balozi Mej. Jen. (Mst) Jacob Kingu alimtembelea Rais wa Kamati za Olimpiki Barani Afrika (ANOCA) Bw. Mustapha Berraf katika Ofisi zake jijini Algiers tarehe 16 April, 2023. Viongozi hao walizungumzia umuhimu wa Kuwendeleza Ushirikiano katika Sekta ya Michezo na Kubadilishana Uzoefu kwenye Kada ya Madaktari wa Michezo pamoja na Kuratibu Mechi za Kirafiki kati ya Tanzania na Algeria.