Tarehe 14 Aprili, 2026. Mhe. Balozi Njalikai alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Samuel Kaveto Mbambo, Balozi wa Namibia nchini Algeria kwa ajili ya kusalimiana (courtesy call).

Pamoja na mambo mengine wawili hao, walijadili masuala ya ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na Namibia.

Aidha, walibadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali ya kikanda na Kimataifa na kutilia mkazo umuhimu wa kuendeleza umoja na mshikimano wa umoja wa Mabalozi wa Nchi za SADC nchini Algeria.