Leo tarehe 21 Aprili 2025, Mhe. Balozi Iman Njalikai amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi Maj. Jen. Ibuge, Mkuu wa Chuo cha NDC katika Ofisi za Ubalozi jijini Algiers.

Mhe. Balozi Maj Jen. Ibuge yupo ziarani nchini Algeria akiongoza ujumbe wa Wanafunzi wa NDC ambao wamekuja katika ziara ya kimafunzo.

Kupitia kikao hicho. Mhe. Balozi Maj Jen Ibuge alitumia fursa hiyo kuushukuru Ubalozi kwa mapokezi mazuri pamoja na uratibu mzima wa ziara kwa kushirikiana na wenyeji.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Njalikai ameishukuru NDC kwa kufanya ziara ya kimafunzo nchini Algeria na kusisitiza umuhimu wa kutumia uhusiano imara na wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili hizi kuendeleza ushirikiano wa kisekta kwenye mafunzo mbalimbali.