Mhe. Iman S. Njalikai, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, alikutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Phanuel Habimana, Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Algeria tarehe 23 Oktoba, 2025 katika Ofisi za Ubalozi jijini Algiers.
Wawili hao walijadili kuhusu ushiriki wa Tanzania kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa Afrika kuhusu uzalishaji wa ndani wa dawa na technolojia za afya unaotarajiwakufanyikaAlgiers tarehe 27 hadi 29 Novemba2025.
Vilevile, walikubaliana kushirikiana katika kufanikisha agenda ya WHO- Afrika kupunguza utegemezi wa uagizaji dawa na vifaa tiba kutoka nje ya bara la Afrika kwa kuimarisha uzalishaji wandani.


