Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman S. Njalikai, leo tarehe 29 Novemba 2023 alitembelea Maonesho ya Kimataifa ya Kuchakata taka na Kuongeza thamani yaliyoandaliwa na Chemba ya Biashara ya Algeria kwa Kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Utunzaji Taka. Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba 2023 jijini Algiers. 

Aidha, Mhe. Balozi alikutana na kuzungumza na Rais wa Chemba ya Biashara wa Algeria, Bw. Kamel Hamenni na Kujadili kwa pamoja hatua ya Utekelezaji wa Makubalino ya Kuanzisha Baraza la Pamoja la Wafanyabiashara wa Tanzania na Algeria ambalo tayari  makubaliano yake yalisainiwa mwezi Agosti mwaka huu. 

Sambamba na hilo, Mhe. Balozi alitembelea Mabanda mbalimbali ya Maonesho likiwemo banda la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambapo alikutana na Mwakilishi kutoka Tanzania Bw. Adrian Kayombo.