Tarehe 3 Februari 2026, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai alimtembelea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Marafiki wa Mapinduzi ya Algeria, Mzee Noureddine Djoudi katika ofisi za Jumuiya hiyo jijini Algiers.

 

Mzee Djoudi ni Balozi wa kwanza wa Algeria nchini Tanzania mwaka 1963 wakati bado ikiwa Tanganyika. Balozi Djoudi alifanya kazi kwa karibu na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika kujenga uhusiano imara kati ya Algeria na Tanzania pamoja na kufanikisha harakati za ukombozi wa Mataifa ya Kusini mwa Afrika.

 

Katika ziara yake hiyo, Mhe. Balozi Njalikai alimkabidhi Balozi Djoudi picha ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambae alikuwa Rafiki Mkubwa wa Algeria.