Katika juhudi za kuendeleza ushirikiano na Algeria katika sekta ya kilimo, Mhe. Balozi Iman S. Njalikai ametembelea kiwanda cha Serikali cha Mbolea cha ASMIDAL kilichopo Jijini Annaba. katika ziara yake hiyo, Mhe. Balozi alikutana na uongozi wa kiwanda hicho na kuona namna bora ya kushirikiana na Tanzania katika eneo la mbolea.



