Tarehe 24 February 2026, Mhe. Iman Njalikai, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, alikutana na kufanya mazungumzo na, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria, Mhe. Boualem Chebihi kwenye ofisi za Wizara hiyo jijini Algiers.
Kikao hicho kilikuwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa maandalizi ya mkutano mkuu wa 6 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano unaotarajiwa kufanyika Tanzania mwaka huu kati ya mwezi Machi hadi Juni 2026.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walikubaliana kuendelea na maandalizi ya jukwaa la kibiashara kati ya Algeria na Tanzania ambalo litaenda sambamba na kuzinduliwa kwa Baraza la Pamoja la Wafanyabiashara wakati wa mkutano huo wa 6 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano.
