Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman S. Njalikai leo tarehe 23 Novemba 2023 alikutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abadalla katika ofisi za Ubalozi jijini Algiers. Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar yupo ziarani kikazi nchini Algeria kwa ajili ya kuhudhuria Mjadala wa Mahakama ya Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Abdelatif Rahal (CIC) jijini Algiers kuanzia tarehe 20 hadi 22 Novemba 2023.