Mhe. Balozi Iman S. Njalikai alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika , Jaji Iman Aboud ambaye yupo ziarani kikazi nchini Algeria. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za Ubalozi jijini Algiers tarehe 19 Novemba 2023.