Mheshimiwa Balozi ameendeleza Mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Taifa la Wamiliki wa Hoteli nchini Algeria Bwana Ahmed Ouldbachir. Viongozi hao wamezungumzia namna ya bora ya Kuimarisha Mashirikiano ya Biashara ya Utalii na Uwekezaji kwa maslahi ya nchi zote mbili.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho ameeleza kuwa Ujumbe wa Shirikisho upo tayari kwenda Tanzania kwa ajili ya Ziara ya Kikazi na Kusainiana Makubaliano ya Mashirikiano ya Utalii na Tanzania mara baada ya Hali ya Corona Kutengemaa nchini Algeria.
