Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mej Jen. (Mst) Jacob Kingu alifanya Mazungumzo na Balozi wa Russia nchini Algeria, Mhe. Valerian Shuvaev katika Afisi za Ubalozi Jijini Algiers tarehe 03/04/2023. Viongozi hao walizungumzia Masuala mbali mbali ya Mashirikiano kati ya Nchi hizi mbili likiwemo suala zima Kukuza Ushirikiano wa Diplomasia ya Watu pamoja Kuongeza Nguvu kwenye Sekta ya Utalii.

