Leo tarehe 6 Machi 2025, Mhe. Balozi Njalikai amewapokea Mabalozi wa nchi za SADC katika ofisi za Ubalozi kwa ajili ya Kikao cha kawaida cha Umoja wa Mabalozi wa Nchi za SADC.

Kikao hicho ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda wa Nchi za SADC na kushauriana kuhusu masuala mbalimbali ya kidiplomasia yanayoendelea kwenye eneo la uwakilishi na ukanda wa SADC kwa ujumla.