Mheshimiwa Balozi ametembelea Kiwanda cha Kuzalisha Solar Panel cha Aures Solaire na Kuendeleza Mazungumzo na Kampuni hiyo kuhusu umhimu wa kufanya Ziara ya Kikazi nchini Tanzania Kutangaza bidhaa zao. Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Noucer ameeleza kuwa ipo tayari kwenda kuwekeza nchini Tanzania lakini pia imeomba kukutanishwa na Mamlaka husika za Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa za Soko na kuona Mazingira ya Uwekezaji.



