Mheshimiwa Balozi Omar Yussuf Mzee akiiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika Kamati Maalum  ya Vijana, Utamaduni na Michezo uliyofanyika Mjini Algiers. Mkutano huo ulihudhuriwa Mawaziri wa Michezo, Vijana na Utamaduni kutoka nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika na ulijadili namna ya Kuimarisha Michezo Barani Afrika, Kuwewezesha Vijana wa Kiafrika katika Shughuli za Kimaendeleo na Kujitegemea pamoja na Kulinda Utamaduni na Tunu ya Afrika ikiwemo kukuza Lugha za Afrika kama vile Kiswahili na Kuwalinda Vijana dhidi ya Utandawazi na Mmongonyoko wa Maadili.