Katika Kuendeleza Juhudi za Kutangaza Utalii wa Tanzania nchini Algeria, Mheshimiwa Balozi Omar Yussuf Mzee amefanya Mahujiano na Jarida la Tauba Event nchini Algeria linaloshughulika na Kuhamasisha na Kutangaza Utalii. Katika Mahojiano hayo, Mheshimiwa Balozi ameeleza Vivutio vya Utalii vinavyopatikana nchini Tanzania kama vile Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Zanzibar. Mheshimiwa Balozi pia ameeleza Utamaduni wa Ustaarabu wa Watanzania kama vile Dini, Chakula, Mavazi, Amani na Utulivu uliopo.
Mheshimiwa Balozi pia amemkaribisha Mkurugenzi wa Jarida la Event pamoja na Timu yake kwenda Kutembelea Tanzania ili Kujionea Vuvutio vya Utalii wa Tanzania pamoja Kupata ladha ya Mapishi ya Kitanzania.

