Mheshimiwa Balozi Omar Yussuf Mzee ametembelea Vinu vya Usambazaji Umeme na Gesi vya Shirika la Taifa la Sonelgas ambalo linashughulika na Uzalishaji na Usambazaji wa Umeme na Gesi nchini Algeria. Shirika hilo pia linazalisha Mitambo Kufujia Umeme na Gesi kama vile Turbains. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Balozi amezungumza Wakurugenzi wa Idara za Shirika hilo juu ya Kushirikiana na Shirika la Umeme la Tanzania TANESCO na Shirika la Umeme la Zanzibar ZECO katika Kubadilishana Uzoefu ikiweo kutatua Tatizo la Kukatika kwa Umeme mara kwa mara.
Shirika la Sonelgaz limesema liko tayari kupokea Timu ya Wataalamu wa Sekta ya umeme kutoka Tanzania kwa ajili ya Kubadilishana Uzoefu katika Uzalishaji, Usambazaji pamoja na Matengenezo ikiwemo changamoto ya Kulipatia Suluhuhisho Suala la kukatika kwa Umeme mara kwa mara.

