Mkutano wa Mheshimiwa Balozi na Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara nchini Algeria Elhamel Mernis na Mkurugenzi wa Hoteli ya Hocine. Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Balozi amewaeleza Viongozi hao umuhimu wa Kuwa na Mashirikiano ya Kiuchumi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Biashara na Uwekezaji. Mheshimiwa Balozi amesisitiza kwamba Tanzania imefungua Milango ya Wawekezaji kutoka Nje na Ubalozi utawapa Mashirikiano ya Kutosha kwa atakaekwenda Kuwekeza nchini Tanzania.