Mhe. Balozi Mej Jen. (Mst) Jacob Gideon Kingu alifanya Mazungumzo na Kaimu Balozi wa Burundi Bi. Nadine MUHIMPUNDU katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Algiers.

Kupitia kikao hicho, Viongozi hao walibadilishana Mawazo kwenye Maeneo mbalimbali  ya Ushirikiano  wa Kidiplomasia kati ya Nchi mbili na Ushirikiano wa  Kikanda ikiwa ni pamoja na Kuimarisha Diplomasia ya Uchumi.

Pichani Mhe. Balozi Mej Jen. (Mst) Jacob Gideon Kingu akiwa na Kaimu Balozi wa Burundi Bi. Nadine MUHIMPUNDU baada ya Kikao cha Courtesy Call tarehe 16-02-2023.