Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman S. Njalikai alishiriki katika Ufunguzi wa Mkutano na Maoenosho ya Nishati ya Afrika ya Kaskazini (NAPEC) na kukutana na Wawekezaji muhimu wa Sekta ya hiyo.
Aidha, Balozi Njalikai alitumia fursa hiyo kuwaeleza Wawakezaji fursa zilizopo nchini Tanzania kwenye eneo la nishati na kuwakaribisha kutembelea Tanzania ili kujionea wenyewe mazingira rafiki ya uwekezaji na biashara. Miongo mwa Wawekezaji hao ni pamoja na Kampuni ya Magherib Pipe, Kawasaki, Valmet, GISB Electric, Optimal global energy na Skyzon Algeria.
Maonesho hayo yalifanyika katika Mkoa wa Oran kuanzia tarehe 13 hadi 15 Novemba 2023.




