Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria Mheshimiwa Maj Gen. Jacob G. Kingu amemkabidhi Rais wa Shirikisho la Taifa la Maendeleo ya Kiuchumi nchini Algeria Mheshimiwa ROUBAI Nasreddine Mounir Mwongozo wa  Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na TCCIA kuhusu Taratibu za Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania.

Makabadhiano hayo yamefanyika tarehe 9 Disemba, 2020 Ubalozini Mjini Algiers, Aidha, Viongozi hao Wamezungumzia Umuhimu wa kuwa na Mashirikiano ya Kiuchumi baina ya Nchi mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo na Utalii kwa Maslahi ya pande zote mbili.