Mnamo tarehe 30 Novemba, Mheshimiwa Balozi Maj Gen. amesaini Kitabu cha Rambirambi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Niger nchini Algeria kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu wa Nchi hiyo Hayati Mamadou TANDJA aliefariki dunia tarehe 24 Novemba, 2020
Mheshimiwa Balozi pia ametoa Salamu za pole kwa Balozi wa Niger nchini Mheshimiwa Malam Manzo AMINOU na kuwataka wawe na Subira na Uvumilivu. Aidha, Ubalozi wa Tanzania uko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

