Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu akitoa Salamu za pole kwa Balozi wa Kuwait nchini Algeria Mheshimiwa Saoud El Faycal Kufuatia Kifo cha Amiri wa Kuwait Marehemu Sabah Al-Ahmad Al-Jabir Al-Sabah kilichotokea tarehe 30 Septemba 2020. 

Mheshimiwa Balozi ametoa Salamu hizo kwa Ubalozi wa Kuwait baada ya Kusaini Kitabu cha Rambirambi na Kuwatakiwa Wakuweit kuwa na Moyo wa Subira katika Kipindi hiki Kigumu na Mungu Kuirehemu Roho ya Marehemu.