Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu akisaini Kitabu cha Rambirambi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Sudan nchini Algeria kufuatia Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na Mwanasiasa Mkongwe Hayati Sadeq Al-Mahdi aliyefariki dunia tarehe 26 Novemba, 2020.
Mheshimiwa Balozi pia ametoa Salamu za pole kwa Balozi wa Sudani nchini Algeria Mheshimiwa Elabeid Mohamed Elabaid Rahma na Kumueleza namna Ubalozi ulivyoguswa na Msiba huo wa ndugu zetu wa Sudan.

