Katika Kuendeleza Mashirikiano yaliyopo katika ya Jamhuri ya Muungano na Madagascar, Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu amemtembelea Kaimu Balozi wa Madagascar nchini Algeria Bibi Rafalimana Jeannie Berthina katika Ofisi za Ubalozi wa Madagascar nchini Algeria.
Viongozi hao wamebadilishana Uzoefu katika Masuala mbali mbali ya Kimaendeleo yanayohusu Nchi zote mbili na Kuzungumzia Umuhimu wa Kuimarisha Mashirikiano ya Kiuchumi na Biashara kati ya Nchi mbili.

