Mhe. Mej Jen. (Mst) Jacob Gideon Kingu alifanya Mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Algeria, Bibi  Therese Gheziel katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Algiers. Viongozi hao walizungumzia umuhimu wa Kuendeleza Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway  na Afrika kwa ujumla ambao umekuwepo kwa muda mrefu.

Pichani Mheshimiwa Balozi akipokea Zawadi ya Kalenda yenye Vivutio vya Utalii  kutoka kwa Mhe. Balozi wa Norway.