Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Jacob G. Kingu amekutana na Kufanya Mazungumzo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SKY ZON ENERGY Barani Afrika Bwana Aissa BAHMIDA. SKY ZON ENERGY imefungua Tawi lake nchini Tanzania kwa Kushirikiana na SUMA JKT.
Mheshimiwa Balozi amewapongeza SKY ZON ENERGY kwa hatua ya Kufanya Uwekezaji katika Sekta ya Nishati nchiniTanzania. Aidha, Mheshimiwa Balozi amemuomba Meneja Mkuu Kuharakisha Kupeleka Timu ya Wataalamu kutoka Algeria kwenda Tanzania kwa hatua za Ufungaji wa Mitambo katika Mradi huo ili uweze Kuanza Kufanya Kazi.

