Mheshimiwa Balozi Maj Gen. Kingu alikutana na Kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa  SAIDAL, Bibi Fatoum Akacem. SAIDAL ni Kiwanda cha Serikali cha Uzalishaji wa Dawa za Binadamu pamoja na Chanjo ya Uviko - 19 ya SINOVAC kwa Kushirikiana na China.

SAIDAL ilianza Kutengeneza Dawa za Binadamu  mwaka 1982 na hadi sasa inazalisha zaidi ya aina 200 za Dawa za Binadamu ambazo zinatumika katika Soko la ndani na Nje ya Algeria. 

Aidha, Mheshimiwa Balozi aliishauri SAIDAL Kuangalia Uwezekano wa Kuwekeza na Kuuza bidhaa zao nchini Tanzania pamoja na Kubadilishana Uzoefu na Tanzania  katika suala zima la Uzalishaji wa Dawa za Binadamu na Chanjo. Kupitia Mkutano huo, SAIDAL imeonesha Nia ya kuwa na Mashirikiano na Taasisi za Serikali na Binafsi za Tanzania pamoja na Kuwapatia Nafasi za Mafunzo ya Vitendo Wanafunzi  wa Kitanzania waliopo Algeria katika kada ya   “Pharmacy” na "Pharmaceutical Industry" kwa lengo la Kuwajengea Uwezo.